Yamoto Band Kutumbuiza Ufini

Bendi maarufu ya vijana wa kitanzania ijulikanayo kama Yamoto Band, itafanya ziara yake barani Ulaya, na baadhi ya nchi watakazo fanya maonesho ya nyimbo zao ni hapa Ufini.

Kwa mujibu wa ratiba yao, wanatawasili Finland tarehe 26 Januari 2017 saa saba mchana wakitokea nchini Tanzania, baada ya ratiba zingine za awali, watafanya onesho siku ya tarehe 28 Januari 2017 huko mjini Tampere Finland. Kwa maelezo zaidi tembelea ukurasa wa Facebook wa FestAfrica.

Jumuiya ya Watanzania Finland inawakaribisha sana watanzania wenzetu hapa Ufini, na pia kutoa mwito kwa Watanzania tuliopo Ufini, kuitumia nafasi hii kupata burudani kutoka NYUMBANI. Maana ni mara chache sana kupata nafasi za kuburudishwa na wazawa wenzetu kutoka nchini kwetu. Karibuni sana.

2017-02-01T23:16:53+00:00January 26th, 2017|habari, Tanzania|Comments Off on Yamoto Band Kutumbuiza Ufini