Vidokezo Muhimu Kuhusu Sherehe Za Miaka 56 ya UHURU Wa Tanzania

Karibu tusherehekee kwa pamoja sherehe za miaka 56 ya uhuru wa Tanzania.

Makala hii inalenga kukupa vidokezo muhimu na taarifa zake kuhusu maandalizi na mambo muhimu kuelekea sherehe za uhuru wa tanzania hapa Ufini.
ATF imejikita katika kuhakikisha inaandaa sherehe zenye urasmi na hadhi ya mtanzania.

Ili kufaidika na utaratibu mzima wa sherehe za mwaka huu, hakikisha umefanya na kufahamu yafuatayo.

Jiandikishe kuhudhuria

Kamati ya Maandalizi ya sherehe inapenda kufahamu idadi ya watu wanaotarajia kuhudhuria sherehe. Hivyo ni muhimu kila mtanzania anaetarajia kuhudhuria sherehe hizi kujiandikisha kupitia tovuti ifuatayo: Fomu ya kujiandikisha kuhudhuria sherehe za Uhuru 2017.

Lipia Chakula Mapema

Katika kuhakikisha kuwa chakula kinaandaliwa cha kutosha kutokana na idadi ya watakaohudhuria, ATF imeweka utaratibu wa Wanajumuia na Wahudhuriaji kulipia chakula mapema. Malipo ya chakula yako kama ifuatavyo:

Kulipia Chakula Mtandaoni Ukumbini
Mtoto Euro 5 Euro 7
Mlipa ADA Euro 8 Euro 13
Asiyelipa ADA Euro 10 Euro 15

Tafadhali tembelea Duka la Mtandaoni la ATF ili upate kununua chakula kwa bei nafuu na kuiwezesha ATF kuandaa chakula kizuri na cha kutosha idadi ya wahudhuriaji. Kila Mtanzania ana haki ya kuhudhuria sherehe za uhuru bila kujali kama amelipia chakula. Malipo ya chakula sio kiingilio cha sherehe.

Vidokezo muhimu:

Muda: 16:15(Saa kumi na robo jioni)
Mahali: Sherehe zitafanyika katika Ukumbi wa Epoon VPK.
Anuani: Itäinen Jokitie 1, 02770 Espoo,
Ramani: Toka Kituo cha Treni cha Espoo Keskus kwenda Ukumbini ni mwendo wa dakika 5 kwa miguu.
Ukumbi: Una uwezo wa kutosha viti 130 pamoja na meza.
Magari: Kuna nafasi 15 za kuegesha magari ambazo zitatumika na wageni waalikwa/rasmi. Kuna sehemu za kuegesha magari zilizo maeneo ya kituo cha treni.
FAQ: Tafadhali tembelea tovuti ya Maswali na Majibu Kuhusu Sherehe za Uhuru
Vazi la sherehe (Dress code): Sherehe hizi ni rasmi, hivyo tafadhali vaa kirasmi.

 

2018-12-05T05:18:37+00:00December 7th, 2017|ATF, habari, UHURU|Comments Off on Vidokezo Muhimu Kuhusu Sherehe Za Miaka 56 ya UHURU Wa Tanzania