Usafiri2019-02-23T01:21:00+00:00

Usafiri Kwenda Opinmäki

Mahali: Ukumbi wa Opinmäen Koulu (Kampus)
Anuani: Lillhemtintie 1, Espoo, FI-02250
Muda: 11:00 (Saa tano kamili asubuhi)
Ukumbi: Auditorium (Kuna nafasi 120 za kukaa).
Magari: Kuna nafasi za kutosha za kuegesha magari.

Jinsi ya Kufika Ukumbini

Toka KAMPPI:
Panda METRO kuelekea MATINKYLÄ (Iso Omena). Kisha ufikapo MATINKYLÄ (Iso Omena), panda Basi namba 532 linaloelekea LEPPÄVAARA au Basi namba 533 linaloelekea JÄRVENPERÄ. Mabasi yote yanaanzia Platform Na. 21. Shuka kituo kiitwacho HENTTAANAUKIO, kisha tembea mita 300 kuelekea Ukumbini, Mtaa wa LILLHEMTINTIE 1. Safari nzima itachukua kama DAKIKA 50.

Toka ISO-OMENA:
Panda Basi namba 532 linaloelekea LEPPÄVAARA au Basi namba 533 linaloelekea JÄRVENPERÄ. Mabasi yote yanaanzia Platform Na. 21. Shuka kituo kiitwacho HENTTAANAUKIO, kisha tembea mita 300 kuelekea Ukumbini, Mtaa wa LILLHEMTINTIE 1. Safari nzima itachukua kama DAKIKA 21.

Toka TAPIOLA:
Panda Basi namba 118 linaloelekea KAUKLAHTI via NIITTYKUMPU (M) toka Platform Na. 44. Shuka kituo kiitwacho HENTTAANAUKIO kisha tembea mita 300 kuelekea Ukumbini, Mtaa wa LILLHEMTINTIE 1. Safari nzima itachukua DAKIKA 27.

Toka ESPOO-KESKUS:
Panda Basi namba 118 linaloelekea TAPIOLA (M) toka Platform Na. 30. Shuka kituo kiitwacho HENTTAANAUKIO, kisha tembea mita 300 kuelekea Ukumbini, Mtaa wa LILLHEMTINTIE 1. Safari nzima itachukua kama DAKIKA 25.

Toka LEPPÄVAARA:
Panda Basi namba 532 linaloelekea MATINKYLÄ toka Platform Na. 11. Shuka kituo kiitwacho HENTTAANAUKIO, kisha tembea mita 300 kuelekea Ukumbini, Mtaa wa LILLHEMTINTIE 1. Safari nzima itachukua kama DAKIKA 30.

Kuja kwa Gari

Kwa wale watakaokuja na usafiri binafsi, basi elekeeni anuani hii LILLHEMTINTIE 1, ESPOO.

Ukumbi wa Mkutano

Maoni

Kamati ya Maandalizi ya sherehe za Uhuru inakaribisha maoni na mapendekezo toka kwa Watanzania wote waishio Finland. Kuwa huru kutuma maoni, mapendekezo na maswali kupitia anuani ifuatayo: mawasiliano@tanfin.org.

Uongozi – ATF