Jumuiya ya Watanzania Finland – ATF, inasikitika kuwatangazia kifo cha Mtanzania
mwenzetu marehemu Daniel Morris Shirima (aliejulikana zaidi kama Ali ).

Marehemu alianguka na kufariki ghafla siku ya Ijumaa ya tarehe 10.05.2019 katika
jengo la maduka la Itä Keskus mjini Helsinki, Finland.

Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kwa ajili ya mazishi huko nyumbani Tanzania
bado inaendelea.

Gharama za kusafirisha mwili ni euro 6000.

Kutokana na gharama kuwa kubwa, tunaomba mchango wako wa hali na mali ili kusaidia
katika kuhakikisha mwili wa ndugu yetu unakwenda kupumzishwa nyumbani, Tanzania.

Tafadhali tuma mchango wako kupitia akaunti ya Jumuiya ya Watanzania Finland – ATF:
Akaunti namba (IBAN): FI22 7997 7997 6161 77
Jina: ATF
BIC: HOLVFIHH
Reference: 1915

Tunatarajiwa tuwe tumekusanya kiwango tajwa hapo juu kabla ya mwezi wa sita.

Hivyo tutashukuru kama utaweza kuchangia au kujitolea kiwango chochote uwezacho hadi
kufikia tarehe 31.05.2019.

Roho ya marehemu ipumzike kwa amani, amina.

Kwa taarifa zaidi wasiliana na:
Bw.Conrad Lyaruu: (Mwenyekiti – ATF) +358 400 762 616
Bw.Edwin Ndaki: (Makamu M/kiti – TDC Global) +358 451 820 920

Au tuma ujumbe kwenye anuani pepe ifuatayo mawasiliano@tanfin.org.

Tafadhali upatapo ujumbe huu mfahamishe na mwingine.

Umoja ni Nguvu

Uongozi – ATF
Mei 16, 2019
Helsinki