Ndugu Watanzania tuishio Ufini

Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Ufini – ATF, kwa masikitiko makubwa unatangaza kifo
cha Mtanzania mwenzetu marehemu Bw Steven Seyayi au Steve, kilichotokea ghafla jijini
Dar es salaam siku ya Ijumaa Novemba 8, 2019 baada ya kuugua kwa muda mfupi. Mauti
yalimkuta njiani wakati wa jitihada za kumfikisha hospitali.

Marehemu aliishi hapa Ufini kuanzia mwaka 2005 hadi 2017 aliporejea nyumbani, Tanzania.

ATF inaratibu ukusanyaji wa mchango wa rambirambi kwa ajili ya pole kwa familia ya
marehemu.

Akaunti namba (IBAN): FI22 7997 7997 6161 77
Jina: ATF
BIC: HOLVFIHH
Ref no: 1931

Tafadhali tumia Ref no: ifuatayo 1931
Ref no: ni muhimu katika utunzaji na ukaguzi wa mahesabu.

Mwisho wa kupokea michango ni Disemba 15, 2019

Kwa taarifa zaidi, tumia anuani pepe mawasiliano@tanfin.org au simu +358 44 240 8110.

Tafadhali, upatapo taarifa hii wajulishe na wengine.

Roho ya marehemu ipumzike milele kwa amani, Amina.

Umoja ni Nguvu
Uongozi – ATF

TANZIA_Steven-Seyayi