Taarifa Ya Msiba

TANZIA

Uongozi wa ATF umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mama Gonga Monica Mfinanga ambaye ni mama mzazi wa Mtanzania mwenzetu John Mfinanga almaarufu OCG.

Msiba umetokea mchana wa tarehe 14 Februari, 2018 huko Arusha,Tanzania.

Imeamuliwa kukutana na kumpa pole ndugu yetu OCG siku ya Alhamisi tarehe 15.02.2018 nyumbani kwake:
Muda: 17:00 (Kumi na moja jioni)
Anuani: Aapramientie 12 B 45 Vantaa.

Mipango ya mazishi bado inaendelea na mtajulishwa siku za usoni.

Kama ilivyo desturi yetu, kutakuwa na mchango wa RAMBIRAMBI kwa ajili ya mkono wa pole kwa Mtanzania mwenzetu John Mfinanga:

Tuma Rambirambi kupitia vielelezo vifuatavyo.
Akaunti: FI 72 1025 3500 2072 64
Benki: NORDEA Bank
Jina: John Mfinanga

Ndugu John (OCG) anatarajia kusafiri kwenda nyumbani Tanzania kuhudhuria mazishi.

Tafadhali mfahamishe na mwingine.

Uongozi – ATF

2018-02-14T18:38:53+00:00February 14th, 2018|ATF, habari, Msiba|Comments Off on Taarifa Ya Msiba