ATF Taarifa ya Mapato na Matumizi 1997-2016

Uongozi ATF kupitia idara ya Hazina inawakilisha taarifa ya Mapato na Matumizi ya ATF kuanzia mwaka 1997 mpaka 2016 Disemba.

Taarifa hii inajumuisha miaka 18 ya Mapato na Matumizi ya Chama ambayo ni tofauti na utaratibu wa kuwa na taarifa kila robo ya mwaka au kila mwaka. Hali hii inatokana na Chama kuwa bwete kwa kipindi kirefu. Baada ya Uongozi mpya kuchaguliwa, taarifa za Mapato na Matumizi zitafuata utaratibu wa kisheria wa mahesabu ya Jumuiya. Taarifa zote zitawekwa kwenye tovuti ya Jumuiya (ATF) ili kuwafahamisha Wanachama na wadau wa ATF kuhusu mapato na matumizi ya Chama.

Endapo kuna swali lolote linohusu Mapato na Matumizi ya Chama, wasiliana na Uongozi kupitia anwani pepe mawasiliano@tanfin.org au hazina@tanfin.org

ATF Taarifa ya Mapato/Matumizi

MUHIMU: Taarifa hii pamoja na nyaraka zingine za ATF zinapatikana kwenye tovuti ya ATF ukurasa wa Nyaraka

Uongozi ATF

2018-12-05T05:18:37+00:00January 18th, 2017|ATF, habari|Comments Off on ATF Taarifa ya Mapato na Matumizi 1997-2016