Sherehe Za Uhuru2018-12-05T05:18:34+00:00

MIAKA 57 ya UHURU wa TanzaniaKila mwaka Tanzania inaadhimisha kumbukumbu ya Uhuru wa Tanganyika uliopatikana tarehe 9 Disemba 1961. Sherehe hizi huadhimishwa kitaifa. Kama jamii ya Watanzania tunaoishi Ufini, mwaka jana (2017) tulisherehekea kumbukumbu ya Uhuru wa nchi yetu, Tanzania, katika sherehe zilizoandaliwa na Jumuiya yetu – ATF.

Sherehe za Uhuru za mwaka huu (2018) zitakuwa ni za pili kuandaliwa na kusimamiwa na sisi wenyewe kupitia Jumuiya yetu (ATF) kwa asimilia 100%. Hivyo ni fahari kwetu kama Watanzania kupata nafasi ya kuonyesha Uhuru wetu, Umoja wetu na Heshima yetu kama jamii kwa kujiandalia na kusimamia vilivyo sherehe za UHURU wetu.

Ni matarajio yetu kwamba, tutafanikisha kuandaa sherehe zenye heshima, na ubora unao shabihiana na haiba yetu Watanzania tunaoishi hapa Finland. Hii ni Jumuiya yetu, na hizi ni sherehe zetu, basi tuzifanye kwa pamoja na kuzipendezesha kwa umoja.

Anuani na Muda wa Sherehe za Uhuru 2018

Mahali: Ukumbi wa Opinmäen Koulu (Kampus)
Anuani: Lillhemtintie 1, Espoo, FI-02250
Muda: 15:30 (Saa tisa na nusu mchana)
Ukumbi: Kuna nafasi 150 za viti pamoja na meza.
Magari: Kuna nafasi za kutosha za kuegesha magari.
Kujiandikisha: Tafadhali jiandikishe HAPA.

Uvaaji/Dress code

Shughuli hii ni rasmi, hivyo kila mmoja anatakiwa kuvaa kirasmi/kiheshima. Pamoja na kuipendezesha sherehe, mavazi rasmi yataipa sherehe heshima na muonekano stahiki.

Mwisho wa kujiadikisha ni tarehe 02.12.2017 saa 23:59


Jinsi ya Kufika Ukumbini

Toka KAMPPI:
Panda METRO kuelekea MATINKYLÄ (Iso Omena). Kisha ufikapo MATINKYLÄ (Iso Omena), panda Basi namba 532 linaloelekea LEPPÄVAARA au Basi namba 533 linaloelekea JÄRVENPERÄ. Mabasi yote yanaanzia Platform Na. 21. Shuka kituo kiitwacho HENTTAANAUKIO, kisha tembea mita 300 kuelekea Ukumbini, Mtaa wa LILLHEMTINTIE 1. Safari nzima itachukua kama DAKIKA 50.

Toka ISO-OMENA:
Panda Basi namba 532 linaloelekea LEPPÄVAARA au Basi namba 533 linaloelekea JÄRVENPERÄ. Mabasi yote yanaanzia Platform Na. 21. Shuka kituo kiitwacho HENTTAANAUKIO, kisha tembea mita 300 kuelekea Ukumbini, Mtaa wa LILLHEMTINTIE 1. Safari nzima itachukua kama DAKIKA 21.

Toka TAPIOLA:
Panda Basi namba 118 linaloelekea KAUKLAHTI via NIITTYKUMPU (M) toka Platform Na. 44. Shuka kituo kiitwacho HENTTAANAUKIO kisha tembea mita 300 kuelekea Ukumbini, Mtaa wa LILLHEMTINTIE 1. Safari nzima itachukua DAKIKA 27.

Toka ESPOO-KESKUS:
Panda Basi namba 118 linaloelekea TAPIOLA (M) toka Platform Na. 30. Shuka kituo kiitwacho HENTTAANAUKIO, kisha tembea mita 300 kuelekea Ukumbini, Mtaa wa LILLHEMTINTIE 1. Safari nzima itachukua kama DAKIKA 25.

Toka LEPPÄVAARA:
Panda Basi namba 532 linaloelekea MATINKYLÄ toka Platform Na. 11. Shuka kituo kiitwacho HENTTAANAUKIO, kisha tembea mita 300 kuelekea Ukumbini, Mtaa wa LILLHEMTINTIE 1. Safari nzima itachukua kama DAKIKA 30.

Kuja kwa Gari

Kwa wale watakaokuja na usafiri binafsi, basi elekeeni anuani hii LILLHEMTINTIE 1, ESPOO.

FAQ: Tafadhali tembelea tovuti ya Maswali na Majibu Kuhusu Sherehe za Uhuru

Picha ya eneo la Ukumbi wa Espoo VPK

Ukumbi wa Shule ya OPINMÄKI, ESPOO – Sehemu zitakapofanyikia Sherehe za Uhuru – 2018

 

Maoni

Kamati ya Maandalizi ya sherehe za Uhuru inakaribisha maoni na mapendekezo toka kwa Watanzania wote waishio Finland. Kuwa huru kutuma maoni, mapendekezo na maswali kupitia anuani ifuatayo: mawasiliano@tanfin.org.

Uongozi – ATF