Ndugu Mwanajumuiya,

Kama ambavyo labda umekwisha kusikia, utoaji wa Pasipoti mpya umeanza nchini Tanzania. ATF inawaletea maelezo rasmi na ya kina ya utaratibu wa kufanya maombi ya kupata Pasipoti za kielektroniki (hasa kwa Wanadiaspora).

Unashauriwa kufanya hivyo endapo hujaomba Pasipoti hii mpya ya kielektroniki tayari. Maelekezo yanapatikana hapa (bofya neno ‘hapa‘).

Endapo utakuwa unahitaji usaidizi wakati wa kujaza fomu ya maombi mtandaoni au kuwa na shida yeyote ya kiuhamiaji, unaweza kuwasiliana na Ofisi za Uhamiaji kupitia anuani pepe:

info@immigration.go.tz

proznz@immigration.go.tz (kwa walioko Zanzibar)

Simu: +255-22-2850575/6 

 

Endapo utakuwa na maswali kwa Uongozi wa ATF kuhusiana na hili, usisite kuwasiliana nasi kupitia anuani yetu pepe ya mawasiliano@tanfin.org

 

Uongozi ATF