Nafasi za Uongozi – 2020

Ndugu Mwanajumuiya,

Kama unavyofahamu kwamba moja ya mada za Mkutano Mkuu wa 2020 ni Uchaguzi wa Viongozi wa Jumuiya yetu.

Uongozi wa ATF unakukaribisha katika mchakato wa maandalizi ya uchaguzi wa viongozi wetu.

Kila Mwanajumuiya mlipa ADA ana haki ya kushiriki katika uchaguzi kwa KUCHAGUA au KUCHAGULIWA katika nafasi ya Uongozi wa Jumuiya.

Hivyo basi, Uongozi wa ATF unakukaribisha kushiriki kwa kutuma JINA lako na NAFASI ya Uongozi ambayo unataka kushiriki.

Zifuatazo ni nafasi za Uongozi wa Jumuiya yetu ambazo unaweza kugombea:
(1) Mwenyekiti
(2) Makamu Mwenyekiti
(3) Katibu
(4) Mjumbe

Tafadhali, tuma ujumbe ulio na JINA lako kamili pamoja na NAFASI ya Uongozi unayotaka kushiriki kwa kupitia namba ya simu ya ATF 044 240 8110 au kwenye anuani ifuatayo mawasiliano@tanfin.org.

ANGALIZO
Ili kushiriki kwenye mchakato wa Uchaguzi, unashauriwa kulipa ADA ya mwaka ya Jumuiya. Suala hili ni sharti la kisheria ambalo lipo kwenye usajili wa Jumuiya.

Hivyo basi, kama bado hujalipa ADA ya mwaka 2020, unashauriwa kulipa ADA ili ushiriki kwenye zoezi la Uchaguzi.

ADA ya mwaka ni EUR 54, lakini ADA hiyo inaweza kulipwa katika mafungu matatu ya EUR 18.50 kwa kila fungu. Senti 50 ni gharama za muamala. Malipo hayo ya EUR 18.50 yanakupa haki ya kushiriki kwenye uchaguzi.
Unaweza kulipia ada ya Uanachama kupitia duka la ATF kwa kuchagua kimojawapo:

  • Kulipa ada kwa mhula mmoja, bofya HAPA
  • Kulipa ada kwa mihula miwili, bofya HAPA
  • Kulipa ada kwa mihula mitatu, bofya HAPA

Rejea KATIBA ya sasa ya ATF

Karibu katika kusaidia kuongoza Jumuiya yetu!

Uongozi – ATF