Nafasi ya kutuma maombi ya pasipoti (sio za kieletroniki)

Ndugu Mwanajumuiya,

ATF imepokea taarifa toka Ubalozi wa Tanzania Uswidi kwamba Afisa Ubalozi wetu anatarajia kuwepo Helsinki kwa ajili ya mkutano wa kiserikali.

Siku za nyuma ATF iliwahi kutuma ombi Ubalozini la kuletewa huduma ya maombi ya pasipoti.

Sambamba na ziara yake ya kiserikali, Afisa Ubalozi amependekeza siku ya JUMAMOSI ya tarehe 28 APRILI, 2018 iwe siku ya kushugulikia maombi ya pasipoti.

Ili kufanikisha zoezi hilo, inabidi wale wote wanaohitaji huduma hiyo wafanye yafuatayo:

UTARATIBU
1. Tuma barua pepe (email) mapema iwezekanavyo kwenda  mawasiliano@tanfin.org

2. Pindi ATF itakapofahamu idadi ya wahitaji wa huduma hiyo, ATF itawataarifu wahitaji muda na anuani ya sehemu litakapofanyika zoezi hilo.

LENGO
Ni muhimu kwa ATF kufahamu idadi ya Watanzania walio na uhitaji ili kuweza kuandaa mazingira mazuri ya kufanya zoezi hilo kwa amani na utulivu, hasa kwa wale watakaokuja na watoto wao.

Kama utakuwa na swali, wasiliana na Uongozi wa ATF kwa kupitia anuani pepe ya mawasiliano@tanfin.org au simu 044 240 8110.

ANGALIZO
Pasipoti hizi zitakazoombwa zitafikia ukomo wake mwaka 2020. Pasipoti hizi si za kielektroniki, ambazo zinaombewa nchini Tanzania.

 

Uongozi – ATF

2018-12-05T05:18:36+00:00April 21st, 2018|Finland, Ubalozi|Comments Off on Nafasi ya kutuma maombi ya pasipoti (sio za kieletroniki)