MWALIKO TOKA JUMUIYA YA ANAMBRA

Jumuiya ya Anambra unawakaribisha Watanzania wote kushiriki kwenye sherehe za Utamaduni wa Mwafrika utakaofanyika siku ya Jumamosi ijayo 11, Agosti, kuanzia saa sita mchana. Kutakuwepo na wawakilishi kutoka nchi kadhaa za Kiafrika wakiwa na maonyesho yao.

Iwapo ungependa kufanya onyesho la kitamaduni siku hiyo wasiliana moja kwa moja na Jumuiya ya Anambra kupitia:

Simu: +358443031191,
Anthony-Claret Onwutalobi (Mwenyekiti wa Jumuiya ya Anambra)
Anuani pepe: chairman@asafinland.org

Sherehe hizo zitafanyika Tikkurila Trio Sport Center (Lantinen Valkoisenlahteentie 52-54, 01300 Vantaa).
Kiingilio kwa watu wazima ni euro 10. Iwapo utashiriki/mtashiriki kama mwaandaji/waandaji wa onyesho la kitamaduni siku hiyo, kiingilio kitakuwa bure.

Baada ya maonyesho tajwa hapo juu kutakuwepo na mwendelezo wa kufurahia siku hiyo:
Mahala: Turkismiehenkuja 6, 00370 Helsinki
Muda: Saa tano mpaka saa tisa usiku wa manane (23:00 – 03:00)

Uongozi ATF
8.8.2018

2018-08-08T21:27:33+00:00August 8th, 2018|Finland, habari|Comments Off on MWALIKO TOKA JUMUIYA YA ANAMBRA