Mkutano Mkuu 20192019-03-22T16:16:49+00:00

Mkutano Mkuu wa ATF – 2019

Tarehe: 23-03-2019
Mahali: OPINMÄKI
Anuani: Lillhemtintie 1, 02250 Espoo
Muda: 11:00 – 18:00

 

Ndugu Mtanzania uishie nchini Ufini,

Jumuiya ya Watanzania waishiao Finland ATF, inakukaribisha kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka (2019).

Mkutano ambao unatoa nafasi ya Kikatiba kwako mwanajumuiya kuchagua au kuchaguliwa kuongoza jumuiya, kupitisha maamuzi yenye tija kwa ustawi wa jumuiya, kupata taarifa ya maendeleo ya jumuiya, makadirio ya bajeti pamoja na taarifa ya mapato na matumizi ya ada yako.

Huu utakuwa ni mwaka wa tatu kufanya Mkutano Mkuu tangu kufufuliwa kwa jumuiya yetu. Katika kipindi hicho yamefanyika mengi, na tumejifunza mengi. Hivyo ni wakati muafaka kutafakari mustakabali wa jumuiya na uwakilishi wake kwako.

MAHALI
Sehemu utakapofanyika mkutano pana mazingira rafiki kwa watoto wa rika zote, pana nafasi za kutosha za maegesho ya magari. Juhudi za makusudi zimefanyika ili kuhakikisha kuwa eneo la Mkutano Mkuu linakuwa na nafasi kwa wanajumuiya wengi kuhudhuria.

AGENDA

  • Kupitisha Muswada wa Katiba
  • Taarifa ya fedha
  • Uchaguzi wa Viongozi Wapya
  • Mfuko wa Msiba
  • Mengineyo

WATOTO

Uongozi umefanya maandalizi yafuatayo kwa ajili ya watoto wetu:
a) Sehemu ya watoto kukaa na kucheza pamoja.
b) Chakula na vinywaji kwa ajili ya watoto.

Hivyo basi, kuweni huru kuja na watoto kwenye mkutano wa Jumuiya yetu.

Ni vema kuja na watoto, kwani itawapa nafasi ya wao kuzidi kufahamiana kama Watoto wa Kitanzania.

UKUMBUSHO
Uongozi unakukumbusha kuweka tarehe hii kwenye kalenda yako, na pia kumbuka kumjulisha Mtanzania mwenzako kuhudhuria mkutano huu.

Katiba ya sasa ya ATF inapatikana hapa

Utaratibu wa kushiriki kuchagua ama kuchaguliwa kuwa kiongozi, unapatikana hapa http://tanfin.org/nafasi-za-uongozi-2019

Umoja ni nguvu.

Uongozi – ATF
23.02.2019