Kuhusu2017-01-22T03:30:37+00:00

 

Jumuiya ya Watanzania Finland

Watanzania waishio Finland walitambua umuhimu wa kufanya shughuli za kijamii kwa pamoja kama Jumuiya, kwa lengo la kujenga uwezo wa kusadiana wao kwa wao. Vuguvugu la kuanzisha Jumuiya ya Watanzania waishio Finland lilianza katikati ya miaka ya 1990.

Mkutano Mkuu wa kwanza wa Jumuiya ulikuwa mwaka 1996. Wanajumuiya waliunda Jumuiya inayoitwa “Association of Tanzanians in Finland ATF Ry” – kwa Kiswahili Jumuiya inatambulika kama Jumuiya ya Watanzania Finland. Jumuiya ilisajiliwa rasmi tarehe 24.02.1998.

Jumuiya inatambua Uhuru, Haki na Usawa wa mtu ambao umeelezwa kwenye katiba ya nchi na sheria zingine. Jumuiya inazingatia Katiba na sheria hizo katika kuunda kundi lenye malengo halali, uwezo endelevu na nia ya kuwa marafiki kati ya Wanajumuiya wenyewe kwa wenyewe, watu na au vikundi vingine vya kijamii.

Jumuiya hii ndicho chombo rasmi cha mawasiliano kati ya Wantanzania waishio Finland na taasisi za Serikali. Vilevile, Jumuiya itakuwa mwenyeji rasmi wa ugeni wowote toka Serikalini au toka Ubalozi wetu wa Uswidi na Balozi zetu zilizo nchi nyingine.