Jumuiya ya Watanzania waishio Finland - ATF inafurahi kukukaribisha kwenye Sherehe za MIAKA 58 ya Uhuru wa Tanzania zilizoandaliwa na jumuiya.
Ili kufanikisha uandaaji wa sherehe hizo, Uongozi wa ATF unakushauri ujiandikishe mapema uwezavyo.
Kujiandikisha mapema kutatoa nafasi kwa Uongozi wa ATF kupanga vema maandalizi ya sherehe hiyo ili kukidhi mahitaji (km chakula, viti, meza, nk) ya idadi halisi ya watakaohudhuria.
Kila mtu anatakiwa kujiandikisha: Mwisho wa kujiadikisha ni tarehe 02.12.2019 saa 23:59 1) Wageni wa Wanajumuiya nao wanahitajika kujaza hii FOMU. Mabadiliko yoyote yatatumwa kupitia namba za simu na anuani pepe zenu.
Orodha ya Chakula (Menu) ni kama ifuatavyo: 1- Pilau plain 2- Biriyani 3- Wali 4- Kuku wa mchuzi 5- Kuku wa kuoka 6- Maharage 7- Kabichi 8- Sambusa 9- Chapati Kama ilivyo ada, kutakuwa na chai, kahawa na vitafunwa vingine baada ya chakula cha jioni.
Sherehe za Uhuru zimeandaliwa kwa gharama za ATF, hivyo basi ATF inategemea ushiriki wa kila mmoja wetu ili kuweka usawa katika kubeba gharama za maandalizi za sherehe zetu za Uhuru.
Watoto wenye umri wa chini ya miaka 7 wataruhusiwa kuingia na kutapata huduma ya chakula BURE. Lakini ni muhimu kwamba waandikishwe ili kufahamu idadi ya watu watakaodhuria.
Ili kufanikisha maandalizi ya sherehe zetu, unashauriwa kulipia gharama za sherehe mapema.
Umechagua kujiunga na Uanachama wa ATF. Kwa kulipa ADA unakuwa umechangia gharama za sherehe. Malipo ya ADA ya Uanachama yanaweza kufanywa kwa AWAMU Moja, Mbili au Tatu. Tafadhali nenda kwenye tovuti ya Duka la Mtandaoni la ATF ambapo utaweza kulipia ADA kwa kiwango ulichochagua.
Umechagua kulipa gharama za chakula kwa njia ya mtandao. Baada ya kubofya sehemu yenye neno TUMA iliyo hapa chini, utapelekwa moja kwa moja kwenye tovuti ya Duka la Mtandaoni la ATF ambapo utaweza kulipia gharama za chakula kwa kadri ya idadi ya watu uliokusudia kuwalipia, yaani watu wazima au/na watoto.
Ni muhimu kuhakikisha kwamba kila mtu utakayemlipia chakula awe amejiandikisha au ameandikishwa kwa kupitia ukurasa huu, kwani kinyume cha hilo, itapelekea mtu huyo kukosa sehemu ya kukaa.