HUDUMA ZA UINGIZAJI NA UTOAJI WA MIZIGO YA DIASPORA NCHINI

Jumuiya ya Watanzania imepokea barua ifuatayo kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Uswidi:

Kwa viongozi wa jumuia ya Watanzania nchi za Nordic na Baltic.
YAH: HUDUMA ZA UINGIZAJI NA UTOAJI WA MIZIGO YA DIASPORA NCHINI
Ubalozi wa Tanzania, Sweden umepokea barua kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambayo ni maelezo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yanayorahisisha utaratibu wa kuingiza na kutoa mizigo ya Watanzania waishio Ughaibuni (DIASPORA).
Maelezo kamili kuhusu utaratibu huo kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambayo yanawasilishwa kwenu yameambatishwa.
TAFADHALI SAMBAZA TAARIFA HII KWA WANA DIASPORA.
“Pamoja Tunajenga Taifa Letu”
Matiku Kimenya
KAIMU BALOZI

 

Kiambatanisho hicho kinapatikana hapa. Tafadhali wajulishe na wengine kuhusu habari hii.

Unaweza kuwasiliana na ATF kupitia: mawasiliano@tanfin.org

2018-01-12T17:54:18+00:00January 12th, 2018|Finland, habari, Tanzania|Comments Off on HUDUMA ZA UINGIZAJI NA UTOAJI WA MIZIGO YA DIASPORA NCHINI