HUDUMA YA PASIPOTI

Ndugu Wanajumuiya,

ATF imepokea taarifa toka Ubalozini kuhusu ujio wa Balozi wetu mpya kuja kuleta hati zake ili kujitambulisha rasmi Serikalini hapa Ufini. Mheshimiwa Balozi atarajiwa kufika siku ya Jumatano 24 (kesho kutwa).

Sambamba na ujio huo wa Balozi, kutakuwa na huduma za maombi ya Pasipoti kwa wale ambao pasipoti zao zimekwisha muda.

ANGALIZO

 1. Pasipoti zinazotolewa ni zile za zamani. Kwa sasa, Pasipoti za kielektroniki zinazotolewa nyumbani
 2. Kumbuka kwamba, Pasipoti za zamani zitaisha kutumika ifikapo Januari 2020.
 3. Afisa Ubalozi bado hajapata hoteli ya kufikia. Ameahidi kuitaarifu Uongozi wa ATF pindi atakapopata uthibitisho wa Hoteli atakayofikia.
 4. Ni muhimu kwa ATF kufahamu idadi ya Wanajamuiya walio na uhitaji ili kuweza kuandaa mazingira mazuri ya kufanya zoezi hilo kwa amani na utulivu, hasa kwa walio na watoto.

UTARATIBU WA MAOMBI

Ili kufanikisha zoezi hili, ni vema kwa wale watakaohitaji hii huduma kufanya yafuatayo:

 1. Tuma ujumbe wa kuthibitisha mahitaji yako mapema iwezekanavyo kwenda mawasiliano@tanfin.org au 044 2408110.
 2. Kuhakikisha kabla ya kuja kwenye shughuli ya maombi ya pasipoti:
 • Uje na risiti ya malipo ya pasipoti SEK 600. Kama pasipoti imepotea itabidi ulipe SEK 1100.
 • Uje na picha tano (5) za “passport size” (urefu 4.5cm na upana 3.5cm). Ziwe za rangi ya maji ya bahari (Sky blue background)
 • Endapo umebadili jina, basi ambatanisha barua ya maelezo ya sababu za kubadili jina na vyeti au hati rasmi zinazo onyesha mabadiliko ya jina lako
 • Kwa mwombaji wa mara ya kwanza mwenye umri wa chini ya miaka 18 (mtoto); maombi yatahitaji cheti cha kuzaliwa cha mtoto na nakala ya pasi ya sasa ya mzazi wa Kitanzania (kama ni Mama au Baba).

Endapo utakuwa na maswali usisite kuwasiliana na Uongozi wa ATF kwa kupitia anuani pepe ya mawasiliano@tanfin.org au simu 044 240 8110

Uongozi ATF

2018-12-05T05:18:35+00:00October 22nd, 2018|Uncategorized|Comments Off on HUDUMA YA PASIPOTI
Array
(
  [type] => 8
  [message] => Undefined variable: undefinedVariable
  [file] => /home/tanfin/public_html/wp-content/plugins/wordfence/lib/wfUtils.php
  [line] => 1524
)