22 08, 2019

TANZIA – Martha Lugora

2019-08-22T06:14:58+00:00August 22nd, 2019|ATF, Msiba|Comments Off on TANZIA – Martha Lugora

Uongozi wa ATF umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kuondokewa na Mama Martha Lugora usiku wa kuamkia tarehe 20.08.2019 katika hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam. Mama Martha Lugora ni Mama mzazi wa mtanzania mwenzetu Bw. Boniface (Bonny) Lugora, na ni Bibi wa Bw. Sydney Lugora. RAMBIRAMBI Kama ilivyo ada yetu hapa UFINI, kwamba pindi [...]

16 05, 2019

TANZIA

2019-05-16T18:59:23+00:00May 16th, 2019|ATF, Msiba|Comments Off on TANZIA

Jumuiya ya Watanzania Finland - ATF, inasikitika kuwatangazia kifo cha Mtanzania mwenzetu marehemu Daniel Morris Shirima (aliejulikana zaidi kama Ali ). Marehemu alianguka na kufariki ghafla siku ya Ijumaa ya tarehe 10.05.2019 katika jengo la maduka la Itä Keskus mjini Helsinki, Finland. Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kwa ajili ya mazishi huko nyumbani Tanzania [...]

21 03, 2019

Watoto nao Wanakaribishwa

2019-03-21T20:59:13+00:00March 21st, 2019|Uncategorized|Comments Off on Watoto nao Wanakaribishwa

Ndugu Mwanajumuiya, ATF inapenda kuwataarifu kwamba, katika Mkutano Mkuu wa ATF utakaofanyika siku ya Jumamosi (23/03/2019), Uongozi umefanya maandalizi yafuatayo kuhusu watoto wenu: Sehemu ya watoto kukaa na kucheza kwa pamoja Chakula na vinywaji kwa ajili ya watoto. Hivyo basi, kuweni huru kuja na watoto kwenye Mkutano wa Jumuiya yetu. Ni vema kuja na watoto, [...]

22 02, 2019

Nafasi za Uongozi wa ATF

2019-02-22T22:45:09+00:00February 22nd, 2019|ATF, habari|1 Comment

Nafasi za Uongozi - 2019 Ndugu Mwanajumuiya, Kama unavyofahamu kwamba moja ya mada za Mkutano Mkuu wa 2019 ni Uchaguzi wa Viongozi wa Jumuiya yetu. Uongozi wa ATF unakukaribisha katika mchakato wa maandalizi ya uchaguzi wa viongozi wetu. Kila Mwanajumuiya mlipa ADA ana haki ya kushiriki katika uchaguzi kwa KUCHAGUA au KUCHAGULIWA katika nafasi ya [...]

20 02, 2019

Mafunzo kwa ajili ya Vijana na Wazazi

2019-02-20T04:11:01+00:00February 20th, 2019|Uncategorized|Comments Off on Mafunzo kwa ajili ya Vijana na Wazazi

Ndugu Mwanajumuiya, Uongozi umepokea taarifa kuhusu kuwepo tukio la kuelimisha vijana, wazazi ambao ni wahamiaji hapa nchini Finland. Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Elimu Finland atakuwepo kwenye tukio hilo. LINI: Alhamisi, Aprili 11, 2019 saa kumi jioni. Taarifa zaidi inapatikana kwenye picha ifuatayo: 🗓 Uongozi ATF