TANZIA – Martha Lugora

Uongozi wa ATF umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kuondokewa na Mama Martha Lugora usiku wa kuamkia tarehe 20.08.2019 katika hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam.

Mama Martha Lugora ni Mama mzazi wa mtanzania mwenzetu Bw. Boniface (Bonny) Lugora, na ni Bibi wa Bw. Sydney Lugora.

RAMBIRAMBI
Kama ilivyo ada yetu hapa UFINI, kwamba pindi mwenzetu anapopatwa na msiba, tuna utamaduni wa kushiriki naye kwa kutoa mkono wa pole ili kuwezesha majukumu ya awali ya tukio husika.

Akaunti: FI22 7997 7997 6161 77
Jina: ATF
BIC: HOLVFIHH
Reference: 1928

KUONANA NA WAFIWA
Bw. Bonny ameondoka 21.08.2019 kuelekea nyumbani, Tanzania.

Utaratibu wa kukutana kwa mkono wa pole utatumwa hapo baadae.

Roho ya marehemu ipumzike kwa amani, Amina.

Uongozi – ATF
21.08.2019

2019-08-22T06:14:58+00:00August 22nd, 2019|ATF, Msiba|Comments Off on TANZIA – Martha Lugora