TAARIFA KWA JUMUIYA

Kwa wanajumuiya nchini Finland/Suomi,

Kuna matukio na taarifa muhimu kwako kujua, na ATF ingependa kukumbusha kuhusiana na taarifa hizo:

  1. Mkutano Mkuu wa mwaka wa Jumuiya ya Watanzania, utakuwa siku ya Jumamosi 3, Machi. Mkutano huo ni saa tano asubuhi mtaa wa Fredrikinkatu 42, Helsinki.
  2. Jiunge kwa kujiandikisha kwenye Jumuiya ya Watanzania (ATF). Ni muhimu kufanya hivyo kupata taarifa zilizo rasmi toka Ubalozini na nchini Tanzania kupitia chombo ambacho kipo tayari Finland kwa manufaa yako na familia yako. Jiandikishe hapa na lipia ada ya Uanachama (ambayo ni euro 54 kwa mwaka). Unaweza kulipia ada hiyo aidha kwa miamala miwili (euro 27, 50 au miamala mitatu (euro 18,50).  Ama sivyo, unaweza kukakamilisha kwa muamala mmoja tu (euro 54). Pesa hizi zinakiwezesha chama chako kuendesha shughuli zake mbalimbali kukutumikia wewe mwanajumuiya. Hii ni lazima kwa ajili ya kuweza kufanikisha shughuli zake ikiwemo upatikanaji wa miundo mbinu kuwasiliana na wanajumuiya, uandaaji na ulipaji wa sherehe za Uhuru wa Mtanzania, na kadhalika.
  3. Kama hujafanya tayari, tunza namba ya simu ya Jumuiya (+358 44 240 8110) kwenye simu yako. Ni muhimu kufanya hivyo kwani huwezi jua lini na wapi utahitaji kuwasiliana na Jumuiya. Vilevile kama mwanachama wa Jumuiya, ATF itaweza kuwasiliana nawe moja kwa moja kupitia mitandao ja jamii kama Whatsapp.
  4. Unaweza kushiriki kama mwanajumuiya, katika kuwania nafasi za Uongozi za ATF. Nafasi tajwa zipo hapa. Unahitaji kujiandikisha kama ilivyodokezwa katika #2 ili uweze kuwania nafasi hiyo. Kujiandikisha inachukua wastani wa dakika tano mpaka kumi na baada ya hapo, utakuwa na nafasi ya kugombea nafasi katika Uongozi.

Kama kawaida, endapo utakuwa na swali kuhusiana na taarifa hii, usisite kuwasiliana nasi kupitia mawasiliano@tanfin.org au simu ya Jumuiya iliyotajwa hapo juu.

2018-03-01T18:49:53+00:00March 1st, 2018|ATF, habari|Comments Off on TAARIFA KWA JUMUIYA