Ndugu Wanajumuiya,

Siku ya Alhamisi Oktoba 25, 2018 Mh Balozi Dr. Willibrod Slaa alikutana na Rais wa Finland Mh Sauli Niinistö kwenye Ofisi za Rais mjini Helsinki, Finland. Mkutano huo ulikuwa wa kujitambulisha rasmi kwa Balozi Dr Willibrod Slaa kama Balozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika nchi za Nordic na Baltic. Tukio la Mh Balozi Slaa kukabidhi barua ya utambulisho lilifuatiwa na sherehe iliyoandaliwa na Rais wa Finland kwa ajili ya Mabalozi wa nchi mbalimbali ambao walijitambulisha siku hiyo.

Ubalozi wa Tanzania Uswidi (Sweden) unaiwakilisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika nchi zifuatazo: Estonian, Denmark, Finland, Greenland, Iceland, Latvian, Lithuanian, Norway, Sweden na Ukraine.

Picha za tukio hilo zimechapishwa kwenye kurasa za Ubalozi wa Kitanzania.

Uongozi – ATF