FAQ2017-11-05T23:05:04+00:00

Maswali na Majibu Kuhusu Sherehe za Uhuru

1. Je, ni lazima kujiandikisha ili kuhudhuria sherehe…?

Suala la kujiandikisha ni lazima, na ni muhimu. Umuhimu wake upo katika zoezi zima la maandalizi ili kufahamu idadi ya watu watakaohudhuria, kwani kutakuwa na sehemu maalumu za kukaa (Viti na Meza), na pia kufuatana na sheria ya matumizi ya kumbi kulingana na uwezo wake, ni lazima tuwe na idadi isiyozidi uwezo wa ukumbi. Hivyo basi ni lazima kujiandikisha kupitia tovuti ifuatayo >> Kuhudhuria Sherehe za Miaka 56 ya Uhuru

2. Je, ni lazima kulipia chakula…?

Kila mhudhuriaji wa sherehe ambaye ni mgeni ama mtanzania asiye mwanajumuiya mlipa ada, atachangia gharama za maandalizi ya sherehe kwa kulipia kiasi cha EURO 12 ikilipiwa mtandaoni, ama EURO 15 ikilipiwa ukumbini. Kumbuka ni lazima kujiandikisha ili kuweza kuhudhuria sherehe hizi. Kila mhudhuriaji atapata chakula. (Watoto umri chini ya miaka 16, wataingia na kupata chakula BURE)

3. Kuna malipo ya aina yeyote ambayo ni kama kiingilio cha sherehe…?

Kila Mtanzania yuko huru kushiriki kwenye sherehe hii. Lakini kutokana na gharama za uandaaji, kila mhudhuriaji ambaye si mwanajumuiya mlipa ada, atachangia kiasi cha EURO 12 ikilipiwa mtandaoni, ama EURO 15 ikilipiwa ukumbini. Kumbuka ili uweze kuhudhuria ni lazima ujiandikishe kuhudhuria sherehe hizi.

4. Nani ni wahusika wakuu wa sherehe hii…?

Hii sherehe ni ya Uhuru wa Tanzania, hivyo basi wahusika wakuu wa sherehe hii ni sisi wenyewe Watanzania. Kwahiyo kila Mtanzania anaeishi hapa Finland anahusika na sherehe hii.

5. Sherehe zinaandaliwa na nani…?

Sherehe zinaandaliwa na kusimamiwa na Jumuiya ya Watanzania Finland – ATF.

6. Sherehe imegharimu au itagharimu kiasi gani…?

Kutakuwa na ripoti ya gharama zote za sherehe. Ripoti hiyo itatolewa siku ya sherehe, na kisha itawekwa kwenye tovuti ya ATF, yaani TANFIN.ORG.

7. Kwa nini gharama ya sherehe ukumbini ni ghali kuliko mtandaoni. Haiwezi punguzwa…?

Kweli gharama za sherehe Ukumbini ni ghali kuliko bei ya Mtandaoni. Lengo ni kuwahimiza watu wafanye malipo  kwa kupitia Duka la Mtandaoni la ATF. Malipo ya mtandaoni yana tija kuu tatu, kwamba:

  1. ATF itafahamu idadi kamili ya watu watakao hudhuria sherehe na pia kupata fedha za maandalizi kwa muda muafaka,
  2. ATF itaweza kutoa zabuni ya huduma ya chakula yenye uhakika na hivyo kuweza kuandaa chakula cha kutosha, na
  3. Kufahamu idadi ya watu, kutasaidia kuepuka tatizo la kutokuwa na chakula kichache au kuwa na chakula kingi.
8. Kwanini mfumo wa kuandaa sherehe umebadilishwa na siyo kama tulivyozoea…?

ATF imeweka jitihada za makusudi za kufanya shuguli zake kwa ufanisi na utaratibu. Hii ni kwa ajili ya kutoa huduma bora na kuandaa sherehe bora zenye hadhi na urasmi unaostahili hadhi ya sherehe za Uhuru.

Hivyo basi, ni lazima kuwa na utaratibu kama ilivyo kwenye taasisi nyingine. Tunahitaji kuandaa sehemu ya kufanyia sherehe yenye nafasi ya kutosha kuhudumia idadi ya watu watakaohudhuria. Ili kulifanikisha suala hilo, ni muhimu kujiandikisha ili ATF ipate makadirio sahihi ya mahitaji ya ukumbi.

Zaidi ya hapo, ili kuandaa chakula cha kutosha (bila kuzidisha au kupunguza), ni lazima ATF iwe na makadirio mazuri ya mahitaji halisi kutoka kwenye idadi ya watu na kisha kulipia chakula mapema.

Ni wazi kwamba hatujawahi kuwa na utaratibu kama huu, kwa sababu ATF kama jumuiya haijawahi kuandaa shughuli yetu wenyewe. Hivyo basi, ni vema kutumia nafasi hii kujifunza kufanya mambo kwa kupanga na kwa utaratibu – na si kwa mazoea.

9. Kwanini tusitumie mitandao ya kijamii kujiandikisha? Mfumo ambao watu wamezoea…?

Utumiaji wa Mitandao ya Kijamii (Social Media) kama Facebook, haitoshi kupata uhakika wa mahudhurio ya watu, kwa kuwa:

  1. Kwenye matukio mengi imekuwa hulka kwa watu kubofya “GOING” lakini pindi ifikapo siku ya tukio husika, mtu huyo anahairisha kwenda.
  2. Pia, si wakati wote majina yanayotumika kwenye Social Media ni majina halisi ya hao wadau.
  3. Facebook haikupi chaguo la kuandika watu ambao utaambatana nao (kama watoto, mke, mme, rafiki, n.k.), endapo utakuwa nao.

Hivyo basi karibu  kujiandikisha kupitia tovuti ifuatayo >> Kuhudhuria Sherehe za Miaka 56 ya Uhuru

10. Je, napataje unafuu/discount kama sisi sote ni Walipa ADA…?

Hivyo basi, kwa Wanajumuiya ambao wamelipa ADA yao ya Mwaka 2019, watanufaika kama ifuatavyo:
i) Wataingia na kupata nafasi za kukaa pamoja na huduma ya chakula bila malipo yoyote ya ziada.
ii) Watoto wao watapata nafasi za kukaa na kupata huduma ya chakula na vinywaji laini bila malipo yoyote ya ziada.

Hivyo basi, ni muhimu kila mmoja wenu atume ujumbe wa WhatsApp au SMS kwenda namba 044 240 8110 au anuani pepe ya mawasiliano@tanfin.org ili kuthibitisha kuhudhuria Sherehe za Uhuru.
Endapo utaambatana na watoto, basi ni muhimu kuwaorodhesha katika ujumbe huo.

11. Naweza kushirikisha mtu au watu wengine katika unafuu/discount wa bei ya chakula…?

Wanajumuiya waliolipa ada ya 2019 wote watahudhuria sherehe bila gharama ya ziada, watoto wote wataingia na kupata chakula bila gharama yoyote. Wengine wote watatakiwa kujiandikisha na kulipia gharama za sherehe kama iliyopangwa.

12. Ninapohitaji kulipia mtandaoni kwa ajili ya zaidi ya mtu mmoja, utaratibu gani unatumika…?

Pindi ufikapo kwenye Duka la Mtandaoni la ATF, unaweza kufanya malipo ya bidhaa nyingi kwa kuanza kuweka bidhaa moja moja kwenye Kikapu/Cart kabla ya kufanya malipo. Kisha baada ya kukusanya bidhaa/manunuzi yako, hapo ndipo unaweza kwenda kufanya malipo ya bidhaaa zote zilizokuwa kwenye Kikapu/Cart.

Hakikisha kila mtu unaemlipia awe amejiandikisha kuhudhuria sherehe ama umemuambatanisha kwenye kujiandikisha kwako

13. Wageni (ndugu, jamaa na marafiki) ambao sio Watanzania wanaruhusiwa?

Ndugu, jamaa na marafiki pamoja na wadau wengine wasio Watanzania wanakaribishwa kushiriki nasi. Ni muhimu wageni hawa kujiandikisha kuhudhuria kupitia tovuti ifuatayo >> Kuhudhuria Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru

14. Sikumbuki namba yangu ya Usajili ya ATF

Tuma barua pepe kwenda  mawasiliano@tanfin.org yenye kichwa cha habari kifuatacho: Nimesahau Namba yangu ya ATF.
Kwenye barua hiyo andika jina lako kamili na namba yako ya simu.
Vielelezo hivyo vitatumika kuthibitisha taarifa zako.